Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

WILAYA YA KILOSA ILIVYOPIGA HATUA KIMAENDELEO KWA MWAKA 2014/15

WILAYA YA KILOSA ILIVYOPIGA HATUA KIMAENDELEO KWA MWAKA 2014/15

Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa wilaya saba mkoani Morogoro yenye wakazi wapatao 438,175 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Mkoa wa Morogoro una wilaya saba ambazo ni Ulanga, Malinyi, Morogoro Vijijini, Kilosa, Gairo, Mvomero and Kilombero.

Ili kupata maendeleo mazuri yenye tija ushirikiano wa watu, chama, kijiji au wilaya huhitajika wakiwemo wadau mbalimbali ili kujiletea maendeleo endelevu.

Katika kujiletea maendeleo, mafanikio na ustawi, halmashauri ya Kilosa imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali kwa hali na mali katika kuleta ustawi katika Nyanja mbalimbali kupitia huduma zao kwa jamii na michango ya kifedha, ambapo miongoni mwa wadau hao ni kampuni ya sukari ya ILOVO, Ofisi ya Rais kupitia wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mafanikio hayo ya mwaka 2014/15 yaliyokuwa kwa 53.38% yanadhihirika wazi hatua za kimaendeleo zilizofikiwa katika sekta mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ikiwemo idara ya afya, maji,elimu msingi, elimu sekondari, kilimo, mifugo na uvuvi, mipango, utawala,ardhi na maliasili, maendeleo ya jamii, usafi na mazingira pamoja na ujenzi.

Miongoni mwa mafanikio hayo ni kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya wazazi kwa ajili ya kusubiria kujifungua katika hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo katika mji mdogo wa Mikumi, kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya maji ikiwemo kutoa huduma ya maji katika vijiji vya Tundu, Kifinga, Iwemba, Msowero na  Lumango, ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule za msingi za Magera katika kata ya Mabula na Twatwatwa katika kata ya Parakuyo,ujenzi wa shule mbili za msingi kwa ufadhili wa Umoja wa nchi za Ulaya EU, ongezeko la madawati 1,422 kutoka madawati… ikiwa jumla ya hitaji ni madawati…… katika shule za msingi 19 pamoja na kuongezeka kwa ufaulu kutoka 44.5% hadi kufikia 52.7% kwa mwaka 2015/16.

Wilaya ya Kilosa pia imefanikiwa katika idara ya elimu sekondari kwa kukamilika kwa vyumba 7 vya madarasa kwa sekondari za Mbumi na  Rudewa, vyumba vya maabara 94 ambavyo vipo hatua za boma na vimepauliwa katika shule mbalimbali za sekondari, ujenzi wa mita 2,330 katika skimu za Mvumi,Rudewa na Mwega, huku sekta ya mifugo na na uvuvi ikikamilisha machinjio mbili za Dumila na Magomeni, ambapo katika sekta ya utawala ikifanikiwa kukarabati ofisi ya mkurugenzi, ununuzi wa magari matatu pamoja na kufanikisha kukamilika kwa uchaguzi mkuu 2015 kwa jimbo la Kilosa lililo chini ya CCM na jimbo la Mikumi chini ya Chadema kupitia Ukawa.

Sambamba na hayo idaraa ya ardhi na maliasili imefanikisha zoezi la kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 20 na idara ya maendeleo ya jamii ikifanikisha utoaji misaada ya vifaa vya shule na ada kwa watoto 350 wa sekondari na 100 wa shule za msingi,Usajili wa vikundi 25 vya vijana na 60 vya wanawake, pia maambukizi ya Ukimwi yamepungua kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 2.5mwaka 2015.

Licha ya mafanikio hayo sekta ya mazingira imefanikiwa ujenzi wa vizimba vitatu vya kukusanyia taka kwa mji wa Kilosa na Ruaha, huku sekta ya ujenzi ikifanikisha matengenezo ya km 28 katika Barabara ya Ulaya –Kisanga na ujenzi wa daraja moja la Berega umekamilika pamoja na ujenzi wa kalvati zenye kipenyo cha sentimeta 90 upande wa barabara ya Tende- Tindiga na tuta limenyanyuliwa mita 2.1 na kuweka changarawe urefu wa km 9.5