Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa

TASWIRA NA MWONEKANO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA

HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA

SURA NA TASWIRA YA HALMASHAURI

1.0   UTANGULIZI:

Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Halmashauri sita za Mkoa wa Morogoro. Halmashauri ilianzishwa mnamo  tarehe 25 Agosti, 1962  chini ya kifungu 6 (1)  cha Sheria za Serikali za Mitaa Sura  333. Baada ya kuvunjwa wakati wa kipindi cha Madaraka Mikoani mwaka 1972, Halmashauri ilirejeshwa tena mwezi Januari 1982.

Halmashauri ina eneo lenye kilometa za mraba 14,245  sawa na 19.5% ya eneo lote la Mkoa wa Morogoro. Halmashauri inatekeleza majukumu yake katika Wilaya za Kilosa na Gairo kufuatia kuanzishwa kwa Wilaya ya Gairo kwa Tangazo la Serikali Na. 73 la tarehe 01 Machi, 2012. Hivi sasa Wilaya ya Kilosa ina eneo la kilometa za mraba 12,393.7 na Wilaya ya Gairo kilometa za mraba 1,851.3 pekee.

Halmashauri ipo kati ya “Latitude” 5o 55’ na 7o 53’ Kusini mwa Ikweta na “Longitude” 36o 30’ na 37o 3’ Mashariki mwa Griniwichi. Halmashauri inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa  upande wa Mashariki na upande wa Kusini  inapakana  na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na Mkoa wa Iringa. Kwa upande wa Kaskazini inapakana na Mikoa ya Manyara (Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto) na Tanga (Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi), na  Magharibi inapakana na Halmashauri za Wilaya za Mpwapwa na Kongwa zilizopo Mkoa wa Dodoma.

2.0   IDADI YA WATU:

Kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 Halmashauri ilikuwa na wakazi 489,513 (Me 244,201 na Ke 245,312) sawa na watu 34 kwa kilomita ya mraba na sawa na 27.8% ya wakazi wote wa Mkoa wa Morogoro. Kwa mwaka 2012 Halmashauri inakadiriwa kuwa na watu wapatao 596,434 ambapo wanaume ni 289,774 na wanawake ni 292,102 sawa  na ongezeko la kila mwaka  2.5%. Halmashauri ilikadiriwa kuwa  na kaya 105,635 zenye wastani wa idadi ya watu 4.6 kwa kila kaya.

3.0 MUUNDO WA UTAWALA WA HALMASHAURI: 

Halmashauri ina tarafa tisa za Mikumi, Gairo, Ulaya, Masanze, Kimamba, Nongwe, Kidete, Magole na Kilosa Mjini. Tarafa hizo zinagawanyika katika Kata 46, Vijiji 164 na Vitongoji 1,040. Halmashauri ina Majimbo matatu ya Uchaguzi na Mamlaka za Miji Midogo mitatu ya Gairo, Kilosa na Mikumi. Serikali imeshatoa Notisi ya kuanzisha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kwa Tangazo la Serikali  Na. 28 la tarehe 31 Agosti 2012.

Halmashauri inapaswa kuwa na jumla ya Waheshimiwa Madiwani 65 wakiwemo Waheshimiwa Wabunge watatu, Waheshimwa Madiwani wa Kata 46 na Waheshimiwa Madiwani viti maalumu 16. Katika Baraza la Madiwani, kuna Waheshimiwa Madiwani wanawake 19 wakiwemo watatu wa kuchaguliwa sawa na 30.6% ya wajumbe. Hata hivyo kwa sasa idadi ya Waheshimiwa Madiwani ni 61 baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Masanze, Mhe. Diwani  Leonard M. Mapunda, kufariki tarehe 05 Julai 2012.

Aidha kuna jumla ya vyama 11 vya siasa ambavyo  ni CCM, SAU, CUF, UDP, NCCR MAGEUZI, JAHAZI ASILIA, CHADEMA, DEMOKRASIA MAKINI, UMD, UPDP na TLP  vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 31 Oktoba 2010. Waheshimiwa Madiwani wote wanatokana na CCM isipokuwa wawili ambao ni wa CHADEMA.

Kwa kuzingatia muundo wa Halmashauri ulioidhinishwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa Waraka Kumb. Na. GA 215/262/0183 wa tarehe 25 Juni, 2012 Halmashauri inazo Idara 13 na vitengo sita kama ilivyo katika jedwali Na. 1.

 

Kwa mujibu wa Ikama ya mwaka 2011/12, Halmashauri ina jumla ya watumishi 4,135 kama ilivyoainisha katika jedwali lifuatalo.

Jedwali Na: 2 Ikama ya watumishi 2011/2012

SN

KADA

IDADI

1

Utumishi na Utawala

226

2

Fedha na Biashara

30

3

Elimu ya Sekondari

597

4

Elimu ya Msingi na Utamaduni

2251

5

Ardhi na Maliasili

32

6

Afya

619

7

Usafi na Mazingira

16

8

Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana

66

9

Maji

51

10

Ujenzi

48

11

Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji

9

12

Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika

139

13

Mifugo na Uvuvi

51

 JUMLA

4,135

Katika Ikama ya mwaka 2012/13 Halmashauri imeomba kuidhinishiwa watumishi 870 ili iweze kutimiza malengo yake kwa ufanisi zaidi.

4.0 DIRA, DHAMIRA NA MALENGO YA HALMASHAURI:

Kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa Halmashauri 2010 - 2015, Dira ya Halmashauri ni “Maisha bora kwa wote”, na dhamira ya Halmashauri ni “Kuipatia jamii huduma na maisha bora kwa kuijengea mazingira mazuri ya ushiriki katika kuleta maendeleo endelevu ya kijamii na uchumi katika Wilaya ya Kilosa”.

Katika kutimiza dhamira yake, Halmashauri imejiwekea malengo makuu manane ambayo ni:

1. Kuboresha huduma ya UKIMWI  na kupunguza  maambukizi mapya.

2. Kuboresha, kuendeleza na kutekeleza kikamilifu Mpango wa Taifa wa Kupambana na Rushwa.

3. Kuimarisha ushiriki wa jamii na watu binafsi katika kupanga, kusimamia na kutekeleza shughuli za maendeleo.

4. Kuendeleza huduma za kiuchumi na miundombinu.

5. Kuimarisha utawala bora na utumishi wa umma katika kuleta maendeleo.

6. Kuimarisha na kuendeleza shughuli za maliasili  na kudhibiti uharibifu wa mazingira.

7. Kuendeleza na kujumuisha masuala mtambuka yakiwemo ustawi wa jamii.

8. Matayarisho ya kujikinga na majanga pamoja na masuala ya dharura.

Halmashauri inao mpango mkakati wa miaka mitano (2010 – 2015).

5.0   HUDUMA ZA KIUCHUMI:

5.1   SEKTA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA:

5.1.1  Kilimo:

Asilimia 88 ya wakazi wa Halmashauri hii hutegemea kilimo kama njia ya kujipatia mapato na chakula.  Malengo ya kilimo kwa msimu uliopita 2011/12 yalikuwa kulima jumla ya hekta 249,618 zikiwemo 206,113 za mazao ya chakula na hekta 43,505 za mazao ya biashara. Hali halisi ya utekelezaji ni kwanba jumla ya hekta 188,919 zililimwa, zikiwemo hekta 158,231 za mazao ya chakula na hekta 30,688 za mazao ya biashara.

Aidha matarajio ya mavuno kwa mazao ya chakula yalikuwa ni kuvuna tani 739,712. Kwa mazao ya chakula na kwa mazao ya biashara yalikuwa ni kuvuna tani 918,138. Hadi mwisho wa wakati wa mavuno jumla ya tani 478,381 za mazao ya chakula na  tani 720,235 ya biashara zilivunwa.

Utekelezaji wa shughuli za kilimo umezingatia maagizo ya Serikali katika kutekeleza Tamko la Kilimo Kwanza na “Fanya Mkoa wa Morogoro kuwa Ghala la Taifa” (FAMOGATA). Shughuli mbalimbali zimefanyika katika kufikia azma hiyo.

Miongoni mwa Shughuli zilizotekelezwa ili kufikia azma hiyo ni:

a) Kuendeleza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

b) Uzalishaji mbegu daraja la kuazimiwa ubora katika vijiji vya Msimba, Malolo, Mwasa, Madudu na Kimamba.

c) Uboreshaji wa skimu za umwagiliaji kwa ujenzi wa mifereji mikuu ya Mwasa (meta 200), Madizini (meta 200), Chanjale (meta 200), Mvumi (meta 2,750 na kalvati 20), Ilonga (meta 2,000 na kalavati 8) na Msowero (meta 2,500 na kalavati 8) pamoja na Mwega kirusha maji (meta 300 x 25).

d) Vikundi vitano vya Mtumbatu, Magubike, Mvumi, Rudewa Gongoni na Ihombwe vimepewa majembe ya wanyamakazi aina ya Mkombozi, pea mbili za maksai na mkokoteni kila kijiji. Pia Wilaya imepokea trekta mpya tatu kutoka SUMA JKT aina ya farmatrack 60 (50 HP2WD) walizokopeshwa wakulima.

Aidha kupitia Serikali Kuu zoezi la kusambaza vocha za pembejeo za ruzuku liliendelea kufanyika. Katika mwaka 2011/2012 Halmashauri ilipata jumla ya vocha 90,776 kama ifuatavyo:

Mapokezi ya vocha za pembejeo yalikuwa kama ifuatavyo:

(a) Mbolea ya kupandia – Vocha 30,242

(b)   Mbolea ya kukuzia – Vocha 30,242

(c) Mbegu (OPV) – Vocha   9,800

(d)   Mbegu (Chotara) – Vocha 18,642

(e) Mbegu (Mpunga) – Vocha 1,800

Hata hivyo jumla ya vocha DAP 3,080; UREA 3,079; OPV 2,906; na chotara 90 hazikutumika na zilirudishwa Wizarani.

Uanzishaji wa Mazao Mapya:

Wilaya imeanzisha uzalishaji wa zao jipya la kakao katika Kijiji cha Kisongwe na tangawizi katika kijiji cha Lumbiji. Hatua iliyofikiwa kwa sasa ni uzalishaji wa tani 96 la zao la  tangawizi.

5.1.2  Umwagiliaji:

Hadi sasa eneo lililoboreshwa kwa ajili ya umwagiliaji ni hekta 11,000 kati ya hekta 32,000 zinazofaa kwa umwagiliaji.

5.1.3  Ushirika:

Halmashauri ina jumla ya Vyama vya Kuweka na Kukopa 55 na Vyama vingine vya Ushirika 21. Wananchi wameendelea kuhamasishwa kujiunga na SACCOS pamoja na vyama vingine vya ushirika. Katika kipindi cha 2011/2012 jumla ya watu 11,827 (Me 7493 na Ke 4334),  vikundi 298 na taasisi 34 zilijiunga na SACCOS na kufanya jumla ya wanachama kuwa 12,159 mwaka 2011. Halmshauri ilitekeleza pia zoezi la uanzishaji wa SACCOS kwa kila Kata kwa 92% na iliendelea na uhamasishaji kwa wananchi ili waendelee kujiunga.

Aidha katika Mpango wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Kukuza Ajira,  SACCOS sita zilifanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya Tsh. 537,000,000 kutoka CRDB; SACCOS nne kupitia Akiba Commercial Bank (Tsh. 79,000,000.00) na jumla ya wajasiriamali 94 walipata mkopo kupitia NMB (T.Shs: 67,120,000.00).

5.2   SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI:

5.2.1  Mifugo:

Ufugaji ni shughuli muhimu inayoendelea katika Halmashauri. Halmashauri ina hekta 483,390 zinafaa kwa malisho. Wanyama wafugwao ni wa asili ambao wanakisiwa kuwa ng’ombe 211,610; mbuzi 92,579; kondoo 24,357; nguruwe 4,917; kuku 500,612; punda 2,941; na sungura 1,201.

Mifumo ya ufugaji inayoendeshwa ni ya aina tatu:-

a) Ufugaji huria ambao ndiyo  mkubwa kwa kundi la ufugaji wa asili katika Tarafa za Magole, Kimamba na Masanze.

b) Ufugaji mchanganyiko wa mifugo ya asili na kilimo cha mazao katika tarafa za Gairo, Nongwe na sehemu ya magharibi ya Tarafa za Magole, Kidete na Mikumi.

c) Ufugaji wa ndani wa ng’ombe na mbuzi wa kisasa  wa maziwa na nguruwe katika Tarafa ya Kilosa Mjini, Kimamba, Ulaya, Mikumi, Magole/Gairo, Kidete na Masanze.

Katika kuendeleza ufugaji shughuli mbalimbali zimeendelea kutekelezwa zikiwemo:

a) Kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na kuhamasisha ufugaji endelevu kwa kutumia madume bora, uhamilishaji na kutoa chanjo.

b)   Kuimarisha miundombinu ya mifugo na kutoa huduma za ugani kwa kuendeleza ujenzi wa miundombinu kama jedwali hapa chini linavyoonesha.

 

Miundombinu ya Mifugo

Na

Miundombinu

Hitaji

Vilivyopo

Pungufu

1

Majosho

164

46

118

2

Minada

13

7

6

3

Vituo vya Afya ya Mifugo

37

4

33

4

Vibanio

55

5

50

5

Machinjio Makubwa

10

6

4

6

Mabanda ya ngozi

10

2

8

7

Mabwawa/ Malambo

46

8

38

c) Kutenga maeneo ya wafugaji ili kupunguza migogoro kwa kuanzisha vijiji vya wafugaji ingawa vijiji vingine zaidi vina mchanganyiko wafugaji na wakulima.

5.2.2  Uvuvi:

Uvuvi katika Halmashauri hufanywa katika mito mikuu 10, mabwawa ya asili na yale yaliyochimbwa na watu binafsi. Kuna jumla ya mabwawa 155 ya kuchimbwa na jumla ya vifaranga 30,000 vya samaki vilisambazwa kwa wananchi katika kipindi cha 2011/2012  ukilinganisha na vifaranga 10,000 mwaka 2005/06

5.3   SEKTA YA ELIMU:

5.3.1  Elimu ya Awali:

Katika mwaka 2011/2012 Halmashauri ilikuwa na jumla madarasa ya elimu ya awali 185 yenye jumla ya watoto 10,969. Kati yao wavulana walikuwa ni 5,542 na wasichana 5,427. Madarasa hayo yapo katika Shule za Msingi 185 ambapo shule 34 hazina madarasa ya awali. Nia ya Halmashauri ni kufanya kila shule ya msingi iwe na darasa la awali.

Idadi ya shule zenye madarasa ya Awali.

Mwaka

Jumla ya shule zote

Shule zenye madarasa ya awali

Shule zisizo na madarasa ya awali

Idadi ya wanafunzi wa awali

WAV

WAS

JML

2011/12

219

185

34

5,542

5,427

10,969

5.3.2  Elimu ya Msingi:

a) Usajili wa wanafunzi Darasa I hadi VII:

Miongoni mwa majukumu makuu ya Halmashauri ni kutoa huduma ya elimu ya msingi kwa wananchi wake na kuboresha huduma hiyo. Katika mwaka 2011/2012, Halmashauri ilikuwa na Shule za Msingi 229 ambapo kati ya hizo 219 ni za serikali na shule tatu  ni za binafsi.  Shule za serikali zilikuwa na jumla ya wanafunzi 103,989 kati yao wasichana ni 53,683 na wavulana ni 50,306 na shule za binafsi zilikuwa na jumla ya wanafunzi 691 ambapo kati yao wavulana ni 331 na wasichana 360.

b)   Uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza:

Katika mwaka 2012 Halmashauri ilifanikiwa kuandikisha jumla wa wanafunzi wa darasa la kwanza 16,617 kati yao wasichana 8,374 na wavulana 8,245 sawa na asilimia 98.5 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 16,870.

b)   Hali ya Walimu:

Halmashauri ina jumla ya walimu 2,213 ikiwa na upungufu wa walimu 386 kulingana na mahitaji ya walimu 2,599. Uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 48 (1:48)

c) Hali ya Majengo na samani:

Kwa mwaka 2011/2012 Halmashauri ilikuwa na vyumba vya madarasa 1,391 kati ya mahitaji ya madarasa 2,599 kukiwa na upungufu wa madarasa 1,124 sawa na asilimia 43.0 ya mahitaji. Vilevile Halmashauri ilikuwa na nyumba za walimu 442 kati ya mahitaji ya nyumba 2,213 kukiwa na upungufu wa nyumba 1.771 sawa na asilimia 80 ya mahitaji. Aidha Halmashauri ilikuwa na matundu ya choo 1,913 kati ya mahitaji ya matundu 5,050 kukiwa na upungufu wa matundu ya vyoo 3,137 sawa na asilimia 62.4 ya mahitaji yote. Aidha kwa upande wa samani Halmashauri ilikuwa na madawati 27,397 kati ya mahitaji ya madawati 46,321 kukiwa na upungufu wa madawati 5,424 sawa na alilimia 34.0 ya mahitaji.

d) Hali ya Vifaa vya kufundishia na kujifunzia:

Katika kukabiliana na tatizo la vifaa vya kufundishia na kujifunzia, Halmashauri ilinunua Vivunge 206 vya mwili wa binadamu, Vivunge 210 vya hesabati na matufe ya ramani ya Dunia 1,470 kupitia mpango wa MMEM. Hata hivyo, juhudi za kupunguza tatizo hilo zinafanyika kwa kuhakikisha kuwa kiasi cha fedha kinatengwa kwenye bajeti kwa ajili ya kununulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

e)   Uwiano wa vitabu kwa wanafunzi:

Halmashauri bado ina upungufu mkubwa wa vitabu mashuleni. Kwa wastani uwiano ni 1:4 ambapo sera inasema kuwa uwiano uwe 1:1.

f)   Hali ya Taaluma:

Hali ya taaluma kiwilaya imepanda. Hii inatokana na jitihada zilizofanyika kwa mazingira ya kufundishia na kujifunzia ambapo hali ya ufaulu kuanzia mwaka 2009 ni kama ifuatavyo:

Mwaka

Waliofanya mtihani

Waliofaulu

%

Me

Ke

Jumla

Me

Ke

Jumla

2009

6434

7161

13595

3400

3135

6535

48.1

2010

5264

6074

11338

3024

6231

9255

54.96

2011

6613

7339

13952

3486

7063

10549

50.6

5.3.3 Elimu ya Sekondari:

Kwa mwaka 2011/2012 Halmashauri ilikuwa na Shule 51 za Sekondari. Kati ya hizo Shule 47 ni za Serikali na shule nne zinamilikiwa na watu binafsi. Katika shule hizi wapo wanafunzi 17,541 kati yao wasichana ni 9,351 na wavulana ni 10,190. Aidha, walimu waliopo ni 625 kati yao walimu wa kike ni 95 na walimu wa kiume ni 526 ambapo mahitaji ya walimu katika shule za sekondari hadi Juni, 2012 ni kama ilivyo katika jedwali:

Mahitaji

Waliopo

ADAM I MGOYI

MKUU WA WILAYA

Kessy J Mkambala

MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA